HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Kinywa Changu, Uhai Wangu: : Kutana na mwanafunzi asiyeona na anayetumia mdomo wake

Huenda umepatana  au kumwona mtu asiye na uwezo wa kuona. Wengi wao hutumia mikono kusoma, wakitumia mfumo wa breli. Hata hivyo, si kila wakati hilo hushuhudiwa. Kutana na  mwanafunzi mmoja, kwa jina Irene Nthambi, kutoka shule ya msingi ya wanafunzi walio na ulemavu wa kutoona huko Thika. Ajabu, kando na kuwa katika hali hiyo, yeye hawezi kutumia mikono yake kuandika, baada ya kupatwa na ugonjwa wa sukari. Hata hivyo, amebuni namna ya kusoma, akitumia mdomo wake. Linaloshangaza, ni namna anavyoandika, na kusoma, na utabaki kumtazama kwa mshangao kuhusu ustadi wake usijue la kusema. Huyu hapa Nancy Onyancha, na maelezo zaidi kwenye makala kinywa changu, uhai wangu.

Show More

Related Articles

Close