HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili Videos

Rhumba La Siasa: Je, hatua ya Ababu na Otuoma kujiuzulu itaathiri kura ya CORD Magharibi mwa Kenya?

Kinara wa CORD na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga anatarajiwa kukita kambi Magharibi mwa Kenya Juma hili kwenye kile ambacho kimeonekana kuwa kujaribu kukinasua chombo ambacho kinasemekana kuenda mrama.

Chama cha ODM kikionekana kupoteza mashiko yake katika eneo hilo huku baadhi ya viongozi waliochaguliwa kwa tiketi ya ODM wakisemekana kuwa mbioni kukihama chama cha Chungwa kuonekana linavunda Magharibi mwa Kenya.

Show More

Related Articles

Close