HabariMilele FmSwahili

Chuo kikuu cha JKUAT Thika chafungwa kwa muda usiojulikana

Chuo kikuu cha JKUAT bewa kuu la Thika ,kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya maandamano ya wanafunzi wanaolalamikia kudorora kwa usalama chuoni humo.

Naibu chansela prof Kinyua amewataka wanfunzi hao kuondoka chuoni humo mara moja. Wanafunzi hao waliokabiliana na polisi,wanawasuta polisi kwa kuzembea kuimarisha usalama wakilalamika kupoteza mali yao mikononi mwa wahalifu.

Vilevile wamelalamikia wahudumu wa bodaboda eneo hilo kushirikiana na wahalifu kuwapora wanafunzi wakiwa wamejihami kwa visu kuanzia mwendo wa saa kumi na mbili jioni.

Kufuatia maandamano hayo msongamano wa magari unashuhudiwa kwenye barabara ya Thika wanafunzi hao wakiziba barabara.

Show More

Related Articles

Close