HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya juu yasitisha utekelezwaji wa kupandishwa kwa ada ya kuegesha magari Nairobi

Mahakama ya juu imesitisha kwa muda utekelezwaji wa kupandishwa kwa ada za kuegeza magari hapa jijini Nairobi.

Jaji James Makau ameamuru kusitishwa kwa hatua hiyo hadi pale kesi iliyowasilishwa na shirikisho la watumizi bidhaa COFEK litakaposkizwa na kuamuliwa.

Makau anasema kesi iliyowasilishwa ina uzito na ipo haja kuangaziwa na mahakama. Wamiliki wa magari ya kibinafsi walitarajiwa kulipa shilingi mia nne kwa siku huku mabasi shilingi 1000.

Hayo yakijiri muungano wa wamiliki wa matatu sasa wanatishia kushiriki maandamano kupinga kuongezwa kwa ada hiyo.Mwenyekiti Simon Kimutai amewataka wahudumu na wamiliki wa magari kutodhubutu kulipa ada hiyo hadi pale mwafaka utakapoafikiwa

Anasema kuongezwa kwa ada hiyo kunalenga kuwanyanyasa wamiliki wa matatu hapa jijini Nairobi ilhali mazingira ya wahudumu wa matatu haijaboreshwa

Show More

Related Articles

Close