HabariMilele FmSwahili

Ada ya kuegesha magari kaunti ya Nairobi yaongezwa

Wamiliki wa magari kaunti ya Nairobi sasa watalazimika kilipia zaidi ada za kuegesha magari kufuatia  agizo lililotoewa na serikali ya kaunti ya Nairobi baada ya kupasishwa kwa sheria ya fedha.

Ujumbe kutoka kwa mkuu wa kitengo  cha kupakia magari  Tom Tinega anasema   unasema wanaopakia magari  kati kati mwa jiji na kwenye barabara ya Kijabe sasa watatozwa  shilingi 400.

Wanaoegesha magari katika  maeneo ya Westlands, Community, Gigiri kilimani, Langata Madaraka  Umoja Kayole Karen Milimani na kadhalika watalipa shilingi 200.

Magari ya kibinafsi yatatozwa  7000 kwa muda wa mwezi na wanaopoteza tiketi zao kulipa shilingi  1000.

Show More

Related Articles

Close