HabariMilele FmSwahili

Baba na bintiye wafariki katika ajali eneo la Fahamuni barabara ya Msambweni- Lunga Lunga kaunti ya Kwale

Mwanamume mmoja wa miaka 40 na bintiye wa miaka 15 wamefariki papo  hapo baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani eneo la Fahamuni katika barabara kuu ya Msambweni -Lungalunga .

Ajali hio imehusisha pikipiki mbili ziligongana ana kwa ana na kusababisha vifo vya wawili hao. Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amethibitisha ajali hio akisema kwamba mwendazake Gabriel Mwero alikuwa amemubeba bintiye Maria Nyamvula Mwero wakielekea shule ya wasichana ya Kingwende ajiunge na kidato cha kwanza kabla ya kukumbana na mauti yao.

Miili ya wawili hao inahifadhiwa katika chumba cha wafu cha hospitali kuu mjini Kwale.

Show More

Related Articles

Close