HabariMilele FmSwahili

Bodi ya dawa nchini yafunga duka 71 za kuuza dawa eneo la Pwani

Bodi ya dawa nchini imefunga duka 71 za kuuza dawa katika eneo la Pwani.

Hii ni baada ya kubainika kuwa duka hizo zimekuwa zikiuza dawa ghushi kwa umma. Dominic Kariuki mkuu wa usambazaji wa dawa anasema oparesheni hiyo ya takriban wiki moja imejiri baada ya uchunguzi wao kubaini dawa nyingi hazijaafikia matakwa ya bodi hiyo

Amesema wameweka mikakati mwafaka katika kila eneo kukabiliana na visa hivyo siku za usoni akitoa wito kwa umma kuwa makini wanapofika katika maduka ya dawa kusaka huduma.

Show More

Related Articles

Close