MakalaMilele FmSwahili

Caroline Mutoko akasirishwa na makala ya ‘Jicho Pevu.’

Wakenya wengi walio kwenye mitandao ya kijamii wameelekeza vidole vya ghadhabu zenye shutuma kali kwa wanahabari wa KTN Mohamed Ali anayefahamika sana kutokana na makala yake ya upekuzi ya ‘Jicho Pevu,’ na mwenzake Dennis Onsarigo. Hii ni baada ya wanahabari hao wawili kutowafurahisha wengi kutokana na upekuzi waliofanya wakipania kuchimbua na kuwamulika haswa waliohusika na mauaji ya mfanyibiashara Jacob Juma. Upekuzi ambao wengi wamelaani wakisema kuwa ulikuwa mbovu na ulikosa utafiti na uanahabari stahiki.
Wakenya hao wameelezea hasira zao wakidai kuwa Ali mwanahabari mtajika sana na mwenzake Onsarigo kwenye upekuzi wao waliangazia sana mwanadada aliyedaiwa kuwa na marehemu Juma usiku aliokumbana na kifo chake, badala ya kuangazia kiini cha kifo chake.
Aliyekuwa mtangazaji wa Kiss Fm Caroline Mutoko amejiunga na wakenya hao katika kuonesha kughadhabishwa kwake na makala hayo. Mutoko amedokeza kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa yeye hufuatilia kwa karibu makala yake Moha walakini makala yake kuhusu kifo cha Juma kimemkera sana kwa kumwanika mwanadada Cheryl Kitonga wazi bila kuzingatia hatari ya kumweka kwa umma mbele ya kamera na kumfichua. Mutoko amedokeza kuwa haikubaliki kamwe katika uanahabari bora kutenda jambo kama lile.

Show More

Related Articles

Close