HabariMilele FmSwahili

Chuo kikuu cha Egerton chafungwa kwa muda usiojulikana

Chuo kikuu cha Egerton kimefungwa kwa muda usiojulikana. Bodi ya chuo hicho imeamrisha kufungwa tawi kuu la chuo hicho pamoja na tawi la Nakuru.

Uamuzi huu unawadia baada ya wanafunzi chuoni humo kuandamana leo na kuharibu mali wakitaka kuruhusiwa kuifanya mitihani yao bila ya kukamilisha karo.

Wanafunzi wamepewa hadi nusu saa ijayo kuondoka chuoni humo.

Show More

Related Articles

Close