MakalaMilele FmSwahili

EVA MWALILI aliponea kifo utotoni…

Kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa sauti yake yenye upekee wa aina yake hutoa nyoka pangoni na kumuelekeza katika himaya kwema za muumba wake. Yaani, kila anapopasua anga za Milele Fm kutoka saa kumi asubuhi hadi saa kumi na mbili, wengi wasiokuwamo katika imani ya uwepo wake Mola wanapomsikia huwa hawana budi ila kunyenyekea na kusujudu kwa msamaha na kuelekeza toba zao kwa Mungu. Anaposikika tu hisia za uwepo wake Mungu husheheni anga kokote unaposikilizia na kupokea Baraka Za Milele kwenye vipindi viwili, cha kwanza kimeelezwa hapa juu kisha kile cha Jumapili. Si mwingine ni yeye tu Eva Mwalili maarufu kwa lakabu yake ‘Mundu wa Ngospol.’
Hata hivyo, wengi wanapomsikiliza na kubadilishwa kutokana na uendeshaji wake wa vipindi hivi kwa umilisi mkuu wa fahamu za neno la Bwana na uwepo wake wa karibu na Mola, kuna vitu ambavyo wengi hawajui kumhusu Eva Mwalili. Hata na walio na ukaribu kwa sana naye hawajui baadhi ya hivi vitu viliwahimkumba na kumkaba koo Mundu Wa Ngospol.
Nimechimba zaidi ya sauti yake tu kutesa kwa baraka anga za Milele Fm ili kukujuza japo angaa kwa kiduchu tu mambo manne makuu hukujua wala kufahamu kumhusu Mundu wa Ngospol.
1.ALIPONEA KIFO UTOTONI;
Wakati mmoja akiwa katika shule ya msingi darasa la nne kuelekea la tano, alijipata katikati ya matunda yaliyoyapendeza macho yake kwa matamanio sio haba, matunda maarufu kwa Kiingereza ‘plums,’ ili upate picha na taswira kamili. Hakupendezwa tu, alichukua hatua na kuamua kuyatundua na kuanza kula na kubugia si moja bali kadri ya yalivyozidi kumpendeza machoni na tayari alikuwa ameyaonja hivyo utamu wake mdomoni na wa kukulia machoni ukampa hamu ya kuzila yale matunda. Si kwamba wingi aliokula ulimtishia uhai wake. Kiasi kilikuwa sawa ila tu mbegu ya mojawapo ya yale matunda ulimsakama na kumkaba koo ukamnyima pumzi za kupumua. Alipotesa fahamu na kugwayagwaya akitafuta hewa ya kupumua asijue ilikuwa kaendapi? Ile mbegu ilikuwa kamnyonga sana maskini mtoto asijue la kufanya ila tu kusubiri kile alichokuwa hana fahamu nacho; Kifo. Ya Mungu ni mengi, jamaa mmoja aliyekuwa akipita akamwona na kugundua kulikuwa na shida na mtoto huyo. Alichukua hatua na kumpa huduma ya kwanza kumpulizia pumzi mdomoni mwake kisha kwa mshtuko wa kupiga chafya akaitema ile mbegu nje. Kufika nyumbani adhabu ya babake ilikuwa ikimsubiri kwa kudhaniwa kucheza zaidi ya kiasi kutokana na babake kutoelewa kilichokuwa kimemsonga mwanawe kutishia kumtoa uhai walakini Mola kamtuma malaika kumwokoa maana alikuwa na mipango ya mengi maishani mwake.
2. HANA FAHAMU NA RANGI yaani yeye ni colour-blind…
Wengi husema wanaume pekee ndio huwa na shida ya kutotambua na kufahamu rangi walakini kumbe labda wakamsahau Mundu wa Ngospol. Yeye amekiri kuwa hutatizika sana kujua rangi hususan zilizo na mchanganyiko. Ni rangi chache tu zisizomtatiza Eva, baadhi zikiwa ni nyeupe na nyeusi tu… zaidi ya hapo ni balaa kwake. Staajabu ya Musa kumbe na ya Firauni hukuwa umeyashuhudia!
3. HUTATIZIKA SANA KUPATA VIATU VINAVYOMFAA VYEMA…
Ilinibidi kupiga tabasamu iliyozaa kicheko punde tu Eva alivyonieleza jinsi na namna anavyosumbuka sana kupata viatu vinavyomtosha miguu yote miwili na kumfaa ahisi ah basi hapa nipo sambamba. Akipata kiatu kimoja kilicho sawa kile kingine huwa lazima kimfinye au kimtatize kwa namna fulani kokote mguuni. Hii ndio sababu kuu imemsababisha Eva kukata kauli ya kupendelea sana viatu huru yaani ‘open’ kuliko vile sitiri yaani ‘closed.’ Anasema ukiingia kwenye sheheni ya viatu kwake ndio mwenyewe utajionea ukweli huo. Duh! Aiseh kumbe bado hata ya Firauni hatukuwa tumeyajua toka huyu mwanake Mola mwenezaji wa baraka milele! Aiyah, haimdhuru, humdhuru tu mwenyewe walakini tunamwombea akombolewe toka hili janga.
4. Ni mwanaTae-Kwondo…
Akiwa katika darasa la nne, akisomea shule ya msingi ya General Kago Primary School, Thika, yeye akiwa na ndugu na rafiki zake wangetoroka masomo ya ziada yaani prep kila saa kumi na kuelekea eneo la Pastoral Centre ili kujifunza TaeKwondo. Ni jambo walizoea kufanya kila wakati mpaka wakawa wanaklabu wa Tae Kwondo japo baadaye walijiondoa labda kwa kupevu zaidi na kukosa muda wa kuelekea kwa mafundisho japo anakiri kwamba anapenda kwa sana na hufuatiliwa sana mchezo huu wa TaeKwondo. Hili ni jambo ambalo anajua hata na wazazi wake hawajui aliwahikufanya. Ala! Hata na mume wake hakujua hili na ndio kwa mara ya kwanza wanapata kujua kupitia makala haya.
Bila shaka ni mambo ambayo labda hatungewahi kwa wakati wote kwenye uhai wetu duniani kama kazi zake Milele Fm hazingetuchochea kumtaka kujua zaidi ya yeye kupasua anga kwa kueneza baraka. Ndiyo hayo sasa, kama hukujua na bila shaka hukujua na umeyajua sasa.
Kazi zake Mola kupitia Eva Mwalili zinashuhudiwa kwa kishindo sana baada ya Mundu wa Ngospol kuteuliwa kuwania mtangazaji bora wa mwaka kwenye tuzo za Groove Awards. Hii ni mara yake ya sita kuteuliwa na atakuwa akiwania kubarikiwa kwa mara ya sita kutwaa tuzo hiyo iliyo na hadhi ya juu sana.
Ili kumpigia kura Eva Mwalili kama Radio Presenter of the year, andika SMS na nano Groove, tenganisha na space kisha andika 14c na utume kwa 811 ili kumfanya Eva Mwalili aendeleze baraka zake Mungu kwenye BarakaZaMilele maana LigiYaWashindi inasheheni baraka tele.
Aidha ili kupigia Gospel Sunday kama Radio Show of the year andika nano Groove, tenganisha na space kisha andika 13b na utume kwa 811 na sote tube washing.

Show More

Related Articles

Close