HabariMilele FmSwahili

Gavana Sonko alazwa katika hospitali ya Kenyatta kwa maumivu ya kifua

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta siku moja tu baada ya kushtakiwa katika mahakama ya Milimani kwa ufisadi wa takriban shilingi milioni 357.

Sonko aliwasilishwa katika hospitali hiyo baada ya kulala korokoroni katika jela la Kamiti Nairobi. Kulingana na mshauri wake wa kisiasa , Sonko alionyesha dalili za maumivu kwenye kifua kutokana na mvutano kati yake na maafisa wa polisi Ijumaa iliyopita

Waakilishi wadi kaunti ya Nairobi wanawataka wenyeji wa Nairobi kuwa watulivu gavana Sonko anapojitetea mahakamani katika kesi za ufisadi zinazomwandama.Gavana Sonko anarejea mahakamani kesho kubaini iwapo ataachiliwa huru au la.

utendakazi katika jumba la City Hall umekuwa wa mwendo wa pole kufuatia hatua ya mahakama kudinda kumwachilia huru gavana Mike Sonko. Ziara ya Milele fm  imebaini wafanyikazi wasio na motisha ya kufanya kazi wengi wakidai kusubiri hatma ya mahakama kesho.

Show More

Related Articles

Close