HabariMichezoMilele FmSwahili

Heineken Yasaini mktaba kufadhili mashindano ya Formula 1

Kampuni ya kinywaji cha Heineken imesaini mkataba wa kufadhili mashandano ya magari ya langa langa(Formula One) kuanzia mwaka huu.Sasa Heineken itakua mfadhili rasmi wa mashinano hayo katika ushirikiano utakaojulikana kama Formula 1 Gran Premio Heineken D’italia 2016.Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo,mkurugenzi wa ubora wa bidhaa za Heineken Gianluca Di Tondo amesema mashindano ya Senior Formula One yameendelea kuwa maarufu ulimwenguni na kwa hiyo Heineken itaendelea kuwaunganisha mashabiki huku wakifurahia kinywaji hicho.Ushirikiano huo utashuhudia idadi ya mashabiki milioni 400 ambao hutazama mashindano hayo duniani kuongezeka kwa viwango vikubwa. Heineken imekua ikijihusisha na ufadhili wa mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA na michuano ya raga ya dunia ambapo sasa inalenga kuendeleza katika mashindano ya Formula One.

Show More

Related Articles

Close