HabariMilele FmSwahili

Idara ya utabiri wa anga yapuuzilia mbali madai ya pwani ya Kenya kukumbwa na kimbunga

Idara ya utabiri wa anga imepuuzilia mbali madai kuwa kimbunga kwa kimombo Cyclone kutoka pwani ya Somalia kitaathiri Pwani ya Kenya na kusababisha mvua kubwa na uharibifu wa mali.

Kulingana na idara hiyo, taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kimbunga hicho sio za kuaminika. Hilo linawadia huku mafuriko yakiendelea kusababisha mahangaiko kwa watu wengi katika sehemu mbali mbali za nchi.

Show More

Related Articles

Close