HabariMilele FmSwahili

Imran Okoth aapishwa rasmi kuwa mbuge wa Kibra

Okoth Benard Otieno almaarifu Imran Okoth ameapishwa rasmi kuwa mbunge wa Kibra. Imran ameapishwa katika kikao cha bunge alasiri ya leo chini ya uongozi wa spika wa bunge la taifa Justin Muturi.

Akiwa amezindikishwa na mbunge mteule Maina Kamanda na mbunge wa Mathare Antony Olouch, Imran amechukua kiapo kuchukua hatamu za uongozi kutoka kwa kakake aliyekuw ambunge wa Kibra Ken Okoth aliyefariki baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu

Show More

Related Articles

Close