HabariMilele FmSwahili

Imran Okoth ndiye mbunge mteule wa eneo bunge la Kibra

Imran Okoth mwaniaji wa kiti cha ubunge wa chama cha ODM ndiye mbunge mteule wa eneo bunge la Kibera. Imran ameongoza katika kura zote zilizohesabiwa katika uchaguzi mdogo uliandaliwa hapo jana kwa kujizolea kura 24636 akifuatwa na mwanaiaji wa chama cha Jubilee Macdonald Mariga kwa kura 11,230, Eliud Owalo wa ANC akipata kura 5,275 huku Khamisi Butichi wa FORD Kenya akiwa na kura 260.Akionyesha furaha yake imran amesema ameridhishwa na matokeo.

Tayari Mariga kupitia mawasiliano kwa njia ya simu amempongeza Imran kwa ushindi huo akisema yuko tayari kushirikiana naye kufanikisha maendeleo.

Hata hivyo wajumbe wa chama cha Jubilee wanadai kushindwa kwa Mariga ni kutokana na vurugu zilzioshuhudiwa wakidai mwaka 2022 watatia juhudi kutwaa kiti hicho.

Akiongea punde tu baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi, Imran akionyesha furaha yake anasema jukumu lake la kwanza ni kuwaunganisha wana Kibra baada ya siasa kali za uchaguzi huo

Nao viongozi wa ODM wakiongozwa na mkurugenzi wao wa uchaguzi Junet Mohammed wanaamini atafanikisha kazi aliyoiacha marehemu Ken Okoth

Wafuasi wake hawakuzuia kuonyesha furaha yao

Show More

Related Articles

Close