HabariMilele FmSwahili

Jamaa aliyeonekana kwenye kanda ya video akimpiga mlinzi wa kike mtaani Komarock akamatwa

Maafisa wa polisi hii leo wamemtia mbaroni  jamaa ambaye aliyeonekana kwenye video akimdhulumu mlinzi mwanamke katika  mtaa wa Komarock jijini Nairobi .

Justus Kamoja mwenye umri wa miaka 30 siku ya jumapili alionekana  akimpiga mlinzi huyo huku ikisemekana kuwa ugomvi ulianza baada ya Justus kukataa kukaguliwa alipokuwa anaingia kwenye lango kuu.

Haya yanajiri  huku dunia inapoendelea na siku 16 za uhamasisho  dhidi  ya dhulma za wanawake.

Show More

Related Articles

Close