MakalaMilele FmSwahili

Je Papa mtakatifu ana mpenzi?

Barua za kuonesha uhusiano wa karibu kati ya papa mtakatifu Pope John Paul II yamefichuliwa. Kwa mujibu wa BBC barua hizo zilizokuwa hifadhi za siri za maktaba ya taifa la Poland kabla ya kufichuliwa, ziliandikiwa mwanamke Mmarekani mfilosofia mzaliwa wa Poland Anna-Teresa Tymieniecka aliyekuwa ameolewa. Kulingana na barua hizo uhusiano huo ulidumu zaidi ya miaka 30.

Uhusiano huo ulianza mwaka wa 1973 Anna-Teresa Tymieniecka alipowasiliana na papa mtarajiwa na aliyekuwa wakati huo kasisi wa Krakow Kadinali Karol [ad id=”186545″]Wojtyla kuhusiana na uandishi fulani wa kifilosofia aliokuwa ameuandika.
Mwanamke huyo wa miaka 50 wakati huo alisafiri hadi Poland kutoka Marekani kwa mkutano wa kujadili uandishi wake na hapo ndipo uhusiano wao wa karibu ulianza kunoga na kuibua hisia tofauti kwani papa na makasisi hawastahili kuwa na uhusuano wowote wa kimapenzi.

Hata hivyo, maktaba ya kitaifa ya taifa la Poland imesema kuwa hakukuwa na lolote la kutia doa uaminifu wa papa mtakatifu Pope John Paul II wakati wa utumishi wake kwa Mungu, kabla ya kufariki kwake mwaka wa 2005.

Show More

Related Articles

Close