BurudaniMilele FmSwahili

Ligi Ya Washindi yakutana Galilaya kwa Baraka Za Milele

Kwa mara nyingine nyota ya jaha yenye baraka si haba imeiangukia familia ya Mediamax. Hii ni baada ya kushinda tuzo tatu za Groove 2016 kwenye hafla iliyoandaliwa Kasarani hapo jana. Milele Fm ilinyakua tuzo mbili zilizokuwa zimeteuliwa kuwania vitengo vyao.

Eva Mwalili mwenye mafuta ya upaku ya kueneza #BarakaZaMilele kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kutoka saa kumi hadi saa kumi na mbili asubuhi na Jumapili saa moja hadi nne asubuhi alishinda tuzo ya mtangazaji bora wa mwaka redioni kwa mara yake ya pili mfululizo, kisha #GospelSunday saa nne hadi saa tisa kikanyakua kipindi bora cha mwaka redioni kwa mara ya sita mfululizo.

Ilikuwa ni siku ya siku kwa hakika hususan baada ya kipindi cha runinga #TheSwitch cha K24 kuwahi tuzo ya kipindi bora cha mwaka kwenye runinga.

Akizungumza kwenye kipindi cha #milelebreakfast Mundu wa Ngospol Eva Mwalili amewashukuru wote waliojitokeza kwa maombi na kura pamoja na kila aina ya jeki iliyosababisha Galilaya kutua mapema katika kituo cha Milele Fm Home of African Hits na ameahidi mengi katika siku za usoni kwa ushirikiano na mtangazaji mwenza Paul Muchesi.

Kutoka kwetu tunasema ahsanteni sana kwa kila mmoja kwa kujituma katika kuhakikisha kuwa sisi sote ni WASHINDI.

Show More

Related Articles

Close