HabariMilele FmSwahili

Mabasi ya Modern Coast yapigwa marufuku na NTSA

Idadi ya waliofariki katika ajali ya barabarani eneo la Salama iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya Modern Coast imefika saba.Kamanda wa polisi kaunti ya Makueni Joseph Ole Napeiyan anasema watu wawili akiwemo dereva na mtoto wa miaka miwili wamefariki hospitalini

Kufuatia ajali hiyo mamlaka ya uchukuzi wa barabarani NTSA imepiga marufuku kuhudumu kwa mabasi yote 88 ya kampuni hiyo.Katika taarifa mkurugenzi George njao anasema kuwa wamesikitishwa na misururu ya visa vya ajali ya mabasi ya kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni.Anawataka maafisa wa polisi kukamata basi la kampuni hiyo litakalohudumu baada ya marufuku hii uchunguzi ukiendelea.

Kufuatia marufuku hiyo wengi wa wasafiri maeneo mbalimbali waliojiandikisha kusafiri na mabasi hayo wamejipata katika njia panda.Wanalalama kuwa usimamizi wa kampuni hiyo umechukuwa muda mrefu kuwaarifu kuhusu marufuku hiyo,wengine wakilazimika kusaka usafiri mbadala.

Hata hivyo usimamizi wa kampuni hiyo umeahidi kushirikiana na kampuni ya Dream Line kusaka usafiri kwa abiria wake,kauli inayoonekana kupingwa na wengi.

Show More

Related Articles

Close