HabariMilele FmSwahili

Mamlaka ya kawi yatangaza kupanda bei ya mafuta

Mamlaka ya kawi nchini imetangaza kupande bei za mafuta ya Petroli, Diesel na mafuta taa kwa senti 70, senti 54 na shilingi 1.64 kwa kila lita moja, mtawalia.

Kufuatia bei hizi mpya Nairobi lita moja ya peteroli itauzwa kwa 110.20, Diesel 102.32 na mafuta ya taa 103.95. Mombasa 108.15, 100.27 na mafuta taa 101.91. Nakuru 109.80, 102.12 na mafuta taa 103.76. Eldoret 110.60, 102.92 na 104.57 kwa lita moja ya mafuta taa. Kisumu 110.60, 102.92 na 104.56 kwa lita moja ya mafuta taa. Bei hizi zinaazwa kutekelezwa saa sita usiku wa leo.

Show More

Related Articles

Close