HabariMilele FmSwahili

Marufuku ya matumizi ya ndege za Dash 8 zinazomilikiwa na Silverstone yafutiliwa mbali

Mamlaka ya uchukuzi wa angani imefutilia mbali marufuku ya matumizi ya ndege za Dash 8 zinazomilikiwa na kampuni ya Silverstone.

Mkurugenzi mkuu Gilbert Kibe anasema Silverstone imetekeleza matakwa yote yaliotolewa na hivyo ndege hizo ni salama.

Agizo hili likiwadia baada ya Silverstone kutangaza kuwafuta kazi baadhi ya wafanyikazi wake wakiwemo marubani katika muda wa mwezi mmoja ujao kutokana na hali ngumu ya uchumi.

Usimamizi wa Silverstone ulidai kwa siku kampuni hii huandikisha hasara ya takriban shilingi milioni 7 kutokana na kusitishwa matumizi ya kwa ndege zake aina ya Dash 8.

Show More

Related Articles

Close