HabariMilele FmSwahili

Makataa yatolewa kwa polisi waliompiga mwanafunzi wa JKUAT kinyama jana kuchukuliwa hatua

Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi na inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai wametoa makataa ya saa 24 kwa polisi waliohusika katika kukiuka haki za wanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT hapo jana wakati wa maandamano kuchukuliwa hatua.

Katika taarifa wawili hao wanasema sheria za polisi ziko wazi na hakuna anayepaswa kukiuka wakitaka uchunguzi wa haraka kuendeshwa baada ya video kusambaa maafisa wa polisi wakimpiga kinyama mwanafunzi hapo jana. Wanasema wote waliohusika lazima watabeba msalaba wao

Show More

Related Articles

Close