HabariMilele FmSwahili

Mbunge Moses Kuria akamatwa kwa tuhuma za kumpiga mwanamke

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amekamatwa. Kwa mujibu wa OCPD wa kituo cha Kilimani Lucas Ogara, Kuria amekamatwa kufuatia tuhuma za kumpiga mwanamke mmoja kwa jina Joyce Wanja katika kampuni ya Royal Media Services tarehe Nane Disemba mwaka jana.

Wanja anadai Kuria alimpiga baada ya kumuuliza kuhusu matamshi aliyoyatoa katika mkutano wa kuchangisha fedha za watoto mayatima kaunti ya Kiambu.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kujibu mashtaka.

Show More

Related Articles

Close