HabariMilele FmSwahili

Mtihani wa KCSE waingia siku ya tatu

Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE unaingia siku yake ya tatu wanafunzi wakitarajiwa kufanya mtihani wa masomo ya kemia karatasi ya pili na kiingereza karatasi ya tatu.

Akiongea mjini Kisii kulikoripotiwa visa vya udanganyifu,waziri wa elimu Prof Goerge Magoha anasema uchunguzi umeanzishwa na washukiwa watakabiliwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Anasema msafara wake mapema hii unaelekea kaunti za Homabay na Migori kutathimi hali kufuatia madai huenda kundi la mtandao unaojaribu kushiriki udanganyifu umeenea hadi maeneo hayo

Shughuli sawia inashuhudiwa na katibu belio Kipsang eneo la mwatate kaunti ya Taita Taveta

Show More

Related Articles

Close