
Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE ukiingia wiki ya pili,wasimamizi wawili wa mtihani huo katika shule ya upili ya wavulana ya Sunshine hapa Nairobi wamesimaishwa kazi kwa madai ya kuchelewa.
Akizungumza baada ya kuzuru shule hiyo mapema leo asubuhi waziri wa elimu profesa George Magoha anasema wizara yake itafuatilia kwa kina mtihani huo kukabili visa vya udanganyifu katika shule hiyo
Magoha vilevile amedhibitisha kisa cha wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana Nyabururu huko Kisii kuzua rabsha hiyo jana Wakati uo huo amedhibitisha kuwa huenda shughuli ya kusahihisha mtihani wa KCPE ukakamilika mwisho wa wiki hii.
Naye katibu wake Belio Kipsanga akiwa kule Naivasha amewataka wasimamizi wa mitihani kuzipanga vyema karatasi za majibu ili kurahisihsa usahihiashaji
Wakati uo huo amesema wataandaa mkutano na wadau wa vituo vya kibinafsi kusaka mbinu ya jinsi ya kuwasajili wanafunzi wao baada ya kubainika vituo hivyo vinahusika pakubwa katika wizi wa mitihani