HabariMilele FmSwahili

Muungano wa wahadhiri wa vyuo vikuu UASU watoa makataa ya wiki moja kushiriki mgomo

Muuangano wa wahadhiri wa vyuo vikuu UASU umetoa makataa ya wiki moja kwa serikali kutekeleza mkataba wa maelewano wa mwaka jana lau washiriki mgomo.

Katika mkao na wanahabari katibu Constantine Wasonga anasema mgomo huo utaanza rasmi tarehe 20 mwezi huu kwani serikali ilikaidi ahadi ya kutekeleza nyongeza ya mshahara kuanzia Novemba mwaka jana.

Anadai hakuna mazungumzo yoyote yatakayoendelea hadi pale serikali itakapowalipa shilingi bilioni 13.8 wanazodai

Show More

Related Articles

Close