HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi ajitia kitanzi baada ya wazazi wake kukosa karo ya kumpeleka shule aliyoitwa Nakuru

Mwanafunzi mmoja anayefaa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu amejitia kitanzi  kwa kukosa kupelekwa katika shule ya upili ya bweni aliyoitwa ya Mama Ngina Kenyatta huko Rongai kaunti ya Nakuru.

Kwa amujibu wa OCPD wa Subukia Edward Imbwaga marehemu Peter Mbugua wa umri wa miaka  16, aliyejizolea alama 352 katika mtihani wa darasa la nane KCPE mwaka jana alidinda kuridhia wito wa kupelekwa shule mbadala baada ya wazaziwe kushindwa kukimu karo ya shule ya Mama Ngina Kenyatta.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya Nyahururu.

Show More

Related Articles

Close