HabariMilele FmSwahili

Mwanamme ajitia kitanzi Mombasa

Mwanamme mmoja amejitia kitanzi huko Mombasa na kisha kuacha ujumbe wa kuwatuhumu ndugu zake anaosema walikosa kumpa msaada.

Mwili wa Kelvin Majiwa  mwenye umri wa miaka 37 ulipatikana ukininginia kwenye nyumba aliyokodi katika mtaa wa zam zam. Majiwa aliacha ujumbe wenye kurasa  6 akielezea jinsi alivyotelekezwa na jamaa zake.

Katika ujumbe huo alioelekeza kwa rafikize na madaktari Majiwa anasema alishindwa kupata hela ya kununua chakula na hata dawa. Anasema tangu alipoanza kuugua ndugu zake wamekuwa wakifuja pesa zao kwa starehe na kukosa kumpa msaada.

Show More

Related Articles

Close