Milele FmSwahili

NHIF yatoa masharti mapya kwa wanachama wake

Hazina ya bima ya afya  NHIF imeweka masharti mapya  yatakayosaidia kuimarisha  utendakazi wake na kuanza kutekelezwa mwezi huu wa Januari.

Ni katika maamuzi yaliyoafikiwa kwenye  mkutano wa bodi  simamizi ya hazina hiyo.mabadiliko hayo  yanalenga kuwaadhibu zaidi wanaokosa  kulipia huduma hizo kwa wakati ufaao.

Wanaokosa kulipa kwa zaidi  ya miezi 12 watahitajika kuanza  upya malipo hayo na kulazimika kusubiri muda wa siku 90 kabla ya kuanza kupokea huduma za matibabu na kulazimika kulipia  ada ya mwaka mmoja mbeleni. Hii ikimaanisha utapoteza hela ulizotozwa masharti

Hayo pia yanawafungia nje walio na zaidi ya mke mmoja  wakitakiwa kusajili mke mmoja pekee kwa   huduma hiyo na watoto 5.

Mabadiliko mengine ni kutakiwa kusubiri kwa muda wa miezi 6 kwa  mwanachama yeyote anayeongezwa baada ya  usajili rasmi ili kuanza kupata huduma. Hata hivyo NHIF inasema  masharti hayo  hayatatumika kwa  wanaofaidi na mipango ya serikali ikiwemo wa Linda Mama, na Inua Jamii.

Show More

Related Articles

Close