HabariMilele FmSwahili

NTSA : Idadi ya wakenya waliofariki kwenye ajali mwaka huu yaongezeka

Wakenya 3,225 wamefariki kupitia ajali za barabarani tangu kuanza mwaka huu hadi sasa.Takwimu za mamlaka ya usalama barabarani NTSA zinaonesha idadi hii imeongeza kutoka 2,827 mwaka jana. Aidha cha kuvunja moyo takwimu hizi zimenyesha wanaotembea kwa miguu ndio wamefariki zaidi ,idadi yao ikiwa watu

Kulingana na takwimu zilizotolewa na mamlaka ya usalama barabarani NTSA, kuanzia mwezi Januari kufikia jana Desemba 2 idadi ya wakenya ambao wameangamia kupitia ajali za barabarani imezidi kwa watu 398 na kufikia watu 3225.

Takwimu hizi zinaonyesha wanaotembea kwa miguu ndio waathiriwa wakuu wa ajali hizi ikiwa waliofariki  mwaka huu pekee ni elfu 1,247, utepetevu wa madereva ikiwa ndio lawama wakenya wamehusisha na ajali hizi.

Tuliozungumza nao katika barabara ya kuelekea Ngara hapa Nairobi, wanasema wengi wa madareva hukosa kufuata sheria za trariki na kuchangia vifo vyao.

Ikiwa wahudumu wa bodaboda ndio wanafuata katika orodha ya waliofariki mwaka huu kwa visa 959, wahudumu hawa wamewasuta wenzao kwa kukosa kuzingatia sheria za trafiki

Kulingana na takwimu hizi abiria waliofariki mwaka huu wamepungua na kufikia 644 kutoka 672 ilivyokuwa mwaka jana,waendesha  baiskeli wakiwa na idadi ya chini zaidi kwa wanaofariki kupitia ajali  barabarani idadi yao kiwa 67.

 

Show More

Related Articles

Close