BurudaniMilele FmSwahili

Rachel Ruto mkewe William Ruto atetemesha mitandao namna alivyompa mkono wa salamu Mwai Kibaki…

Mke wa naibu rais William Ruto mara nyingi huwa hagongi vichwa vya habari na ni mara chache sana huonekana mbele ya umma, jambo linalowavutia wengi na kumuenzi sana. Jumamosi wikendi iliyopita mkewe naibu wa rais alijiunga na wakenya maeneo ya Nyeri kuomboleza na kumpa heshima za mwisho aliyekuwa mama wa taifa bi Lucy Kibaki. Rachel Ruto alipopatana na mstaafu rais Mwai Kibaki, namna alivyompa mkono Kibaki kwa salamu iliwaacha wengi vinywa wazi na kusababisha mitandao ya kijamii kuzua mjadala kuzingira maana ya salamu hizo. Salamu hizo zake mkewe naibu rais kwake mstaafu rais Kibaki zimezungumziwa kuwa ndiyo njia bora na mwafaka unaotumika kumfananisha uwakilishi mwema wa malezi stahiki ya asili ya jamii ya Nandi. Rachel Ruto alidhihirisha wazi jinsi mtu alivyokuzwa na kulelewa kuwaheshimu wakubwa wako kwa salamu za mikono miwili. Kulingana na itikadi za Nandi unapomsalimia mkubwa wako unastahili kutia ladha ya kuinamia mbele huku kichwa kikiwa chaegemea chini japo kwa kiduchu tu kuonesha heshima.

Show More

Related Articles

Close