HabariMilele FmSwahili

Rais aonya wanasiasa wa Jubilee wanaopinga mwafaka wa kitaifa

Rais Uhuru Kenyatta ameapa kuwakabili wanasiasa haswa wa Jubilee wanaopinga jitihada za maridhiano ya kitaifa.

Akizungumza huko Gatundu Kaskazini kaunti ya Kiambu, rais anasema hatawaruhusu wanasiasa hao wanaohusishwa zaidi na naibu wake Dr William Ruto, kuwapotosha wakenya kuhusiana na ripoti ya BBI.

Ni semi hizi ambazo zimemkeera sana,rais Uhuru Kenyatta ambaye sasa anasema hataruhusu tena.

Rais aliyekuwa mwingi wa hasira anadai kuwafahamu wanaopinga ripoti ya BBI na kwamba hataruhusu hilo kuendelea.

Rais aidha anawarai wakenya kutokubali kupotoshwa na wanasiasa na badala yake kujisomea ripoti hiyo aliodai ina mengi kwa manufa aya taifa

Na katika hafla tofauti,huko Makueni, waziri wa usalama Dkt Fred Matiangi alirindima ngoma ya rais,akiwakashifu wanasiasa wanaopinga ripoti hii.

Kulingana na Matiang’i ripoti hii ya jopo la maridhiano ni sharti ifikishwe kwa wakenya walio na uamuzi wa mwisho kuhusiana na mapendekezo yaliomo

Show More

Related Articles

Close