HabariMilele FmSwahili

Ripoti ya BBI  yatolewa rasmi kwa umma

Ripoti ya BBI sasa iko mikononi mwako wewe mkenya kuipiga msasa na kuamua hatimaye yake.Ni baada ya waasis wake Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kuiweka wazi kwa wakenya kwenye hafla iliofanyika katika ukumbi wa Bomas.

Akuweka wazi ripoti hii, Rais amewakumbusha wakenya haikuwa rahisi yeye kuamua kuzungumza na  Raila na kusaini mwafaka wa Machi 9 mwaka jana uliopelekea kuzaliwa ripoti hii.

Rais anasema baada yake kushinda uchaguzi mwaka 2017 alishindwa kuliongoza taifa kutokana na ghasia zilizoibuka hivyo hakuwa na budi kumtafuta Raila wazungumze

Hapa,akiwaonya wanaokosoa ripoti hiyo badala yake akawataka waisome na kutoa maoni yao kabla ya kutekelezwa rasmi siku zijazo

Raila akisema wakenya ndio watakua na usemi mkubwa kuhusu hatima ya ripoti hii

Naye Ruto akielezea kuridhishwa na mapendekezo ya ripoti hiyo amewataka wanasiasa hasa wa upinzani kutobadili msimamo wao

Naye Rais wa Tanzania John Magufuli kupitia hotuba iliosomwa na waziri wa masuala ya kigeni amewapongeza Uhuru na Raila kwa mwafaka wao

Show More

Related Articles

Close