HabariMilele FmSwahili

Simba aliyewahangaisha wakaazi wa Kurgar huko Uasin Gishu anaswa

Mafisa wa  shirika la wanyama pori KWS wamefaulu kumkamata simba ambaye amekuwa akiwahangaisha wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu kwa kpindi cha majuma mawili sasa.

Afisa wa  shirika hilo John Mwakima amedhibitisha kukamatwa simba huyo  mapema leo katika shamba la Kurugar eneo la Moiben na amesafirishwa hadi katika mbuga ya kitaifa  ya ziwa Nakuru.

Simba huyo tayari alikuwa amewaua ng’ombe watatu na wakulima waliopata hasara wanatarajiwa kufidiwa.

Show More

Related Articles

Close