MichezoMilele FmSwahili

Taifa la Urusi lapigwa marufuku ya miaka 4 kushiriki mashindano makuu duniani na WADA

Taifa la urusi limepigwa marufu ya miaka minne ya kutoshriki mashindano makuu duniani kwa sababu ya swala la matumizi ya dawa haramu za kutitimua misuli.

Shirika la kupambana na dawa hizo duniani WADA (World Anti-Doping Agency) limetoa tangazo hilo dakika chahe zilizopita na ina maana kwamba taifa hilo la Urusi halitashiriki mashindo ya Olimpiki mwaka ujao mjini Tokyo Japan sawa na fainali za kombe la dunia za 2022 nchini Qatar.

Licha ya Marufuku hiyo,Urusi itashiriki michuano ya  mwaka ujao kwa sababu UEFA haijaorodheshwa kama mwandalizi wa mashindano makuu duniani.

Waziri wa michezo nchini balozi Amina Mohamed ameonya kuwa huwenda Kenya ikafuata mkondo wa Urusu endapo wanaspoti wa humu nchini wataendelea kuingia katika mtego wa dawa hizo.

Show More

Related Articles

Close