HabariMilele FmSwahili

Taifa linakabiliwa na tishio la uhaba wa chakula takriban kaunti 10 zikivamiwa na nzige

Taifa linakabiliwa na tishio la uhaba wa chakula kufuatia uvamizi wa nzige katika takribani kaunti 10 nchini. Waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri amekiri kuwa serikali inakabiliwa na changamoto ya kuwakabili wadudu hao ambao tayari wamesabisha hasara kubwa mashambani katika  kaunti za Mandera, Wajir, Marbasit ,Garrisa, Isiolo na Samburu.

Kulingana na Kiunjuri serikali imeweka mikakati makhsusi ya kudhibiti uvamizi huo katika muda wa majuma 2 yajayo kupitia kunyunyiza dawa katika maeneo yote yanayoathiriwa.

Hata hivyo Kiunjuri amekanusha madai ya kuwepo nzige kaunti za Meru na Machakos akisema waliopatikana ni panzi.

Show More

Related Articles

Close