HabariMilele FmSwahili

Uchaguzi mdogo eneo bunge la Kibra waanza

Vituo vyote vya kupigia kura vimefunguliwa wenyeji wa Kibra wakiendelea kushiriki zoezi hilo. Uslama umeimarishwa kila mahali shughuli hiyo inapoendelea.

Shughuli ya upigaji kura eneo bunge la Kibra inaendelea kwa utaratibu ufaao foleni ndefu zikishuhudiwa katika vituo mbalimbali.

Mwaniaji kiti cha ubunge wa chama cha ODM Bernard Otieno Okoth maarufu Imran na kinara wake Raila Odinga wanatarajiwa kupiga kura katika shule ya Old Kibra saa nne asubuhi na saa tano asubuhi hii mtawalia.

Hata hivyo wabunge wa vyama mbalimbali ambao pia ni maajenti katika shughuli hiyo wameonyesha kuridhishwa kwao na jinsi shughuli hiyo inavyoendelea

Show More

Related Articles

Close