HabariMilele FmSwahili

Ukumbusho wa shambulizi la Dusit D2 mwaka mmoja baadaye

Ni mwaka mmoja sasa tangu shambulizi la kigaidi la kituo cha biashara cha Dusit D2 eneo la Riverside,jijini Naiobi ambapo watu 21 walipoteza maisha yao huku wengi wakipata majeraha.

Kutolipwa fidia na kuachwa bila kazi ndio hali wanayoishi makumi ya  manusura wa shambilizi la Dusit D2

Wengi waliokumbana na shambulizi hili walikuwa wahudumu wa texi magari yao yaliteketezwa. Nancy Mweu amekutana na mmoja wa wahudumu hawa ambaye pia alikutana na mtutu wa bunduki ya magaidi walioshambulia hoteli hiyo.

Ni saa tisa unusu. Niko katika jengo la Dusit D2 hapa Nairobi. Tarehe kama ya leo mwaka jana hapa singefika……risasi zilisika kila mahali, mabomu yakilipuka, nduru za manusura zikisika katika jumba ninalolitazama chini ya mita 20 kutoka nilikosimama

Charles Kiare ni dereva wa teksi….ananisimulia aliyoyaona saa na siku hii mwaka mmoja uliopita

Kwa kushtuka ananipata uhalisia wa jinsi matukio yalivyotokea sekunde baada ya nyingine.

Kiari baba ya watoto 3 anasema alikutana ana kwa ana na gaidi aliyempiga risasi.

Akishukuru mungu kwa hai hii leo,kinachomkosesha usingizi ni kwamba  kazi yake iliisha siku hiyo. Gari lake la texi liliteketezwa

Yeye na marafiki wake kadhaa walihudumu hapa, magari yao waliyanunua kwa mkopo wa benki……anasema kufikia sasa hajapata mwamko mpya wa maisha

Ananiambia licha ya ahadi ya fidia hakuna mwanga katika ahadi hii akisema mwaka mmoja baadaye na hajui ataanzia wapi.

Kiarie ni miongoni mwa wafanyabiashara walioshiriki biashara mbali mbali eneo hilo ambao mwaka mmoja baadaye hawana kazi wala pa kupata mkate wa kila siku.

Show More

Related Articles

Close