HabariMilele FmSwahili

Usalama waimarishwa eneo bunge la Kibra tayari kwa uchaguzi mdogo hapo Kesho

Usalama umeimarishwa vilivyo eneo bunge la Kibra hapa Nairobi tayari kwa uchaguzi mdogo utakaoandaliwa hapo kesho.

Wenyeji tuliozungumza nao wameelezea furaha walionayo wakisubiri kesho kumchagua anakaye waakilisha bungeni kipindi cha miaka 2 iliyosalia.

Tuliozungumza nao aidha wametoa wito kwa wenzao kudumisha utulivu na amani wakati zoezi hilo litakuwa linaendelea hadi baada ya matokeo kutolewa na tume ya uchaguzi IEBC

Show More

Related Articles

Close