MakalaMilele FmSwahili

Vioja na viroja vya Bernard Ngatia na Boniface Manono …

Kisa cha jamaa mmoja aliyeonekana kwenye video akipokea kichapo cha polisi kipigo kilichomsababishia majeraha na kuripotiwa kufariki hapo jana kimechukua mkondo mwingine. Hii ni baada ya kujitokeza kwa jamaa anayedai kuwa ndiye mwathiriwa aliyeonekana kwenye video hiyo.
Kuchipuka kwa jamaa huyo kwa jina Boniface Manono kimeibua hisia na maoni tofauti na kuzua cheche za maneno kati ya wakenya mtandaoni. Hii ni kutokana na jamaa mhusika mkuu anayefahamika na kutambuliwa na wengi kuhusika katika maandamano kuwa ni Bernard Ngatia wala si Boniface Manono.
Tukio hili limezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii hususan tweeter ambapo waandishi wa blogu tofauti na wakenya mtandaoni wanazamia undani wa nani ni nani kwenye kisa hiki ambacho kinazidi kuzua nipashe nikupashe na nitemee nikutemee safari ya hujui najua zaidi yako mtandaoni.
Boniface Manono amepuuziliwa mbali na wengi wa watu wanaodai kuwa anatumiwa na serikali kuficha ukweli kwamba mhusika mkuu Bernard Ngatia ndiye aliyepigwa na alifariki.
Ni taarifa inayozidi kutukia na tutakudokezea kila sehemu ya matukio na matukizi ya mchipuko huu unaowaacha wengi vinywa wazi.

Show More

Related Articles

Close