HabariMilele FmSwahili

Viongozi mbalimbali wazidi kutilia shaka matokeo ya sensa

Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanazidi kutishia kuelekea mahakamani kupinga matokeo ya shughuli ya sensa hasaa katika maeneo wanayowakilisha. Wa hivi punde ni wabunge wa Kaskazini Mashariki mwa taifa wanaopinga matokeo ya maeneo hayo wakisema idadi iliyotolewa ya watu katika maeneo bunge saba eneo hilo haiwiani na sajili ya wapiga kura.

Duale sasa analitaka shirika la takwimu nchini kufungua mitandao yake ili kuweza kubaini yaliyojiri katika shughuli hiyo nzima

Anasema huenda kuna njama ya baadhi ya maafisa serikalini kupunguza mgao wa raslimali katika eneo hilo akitaka kuelezewa jukumu la viongozi wa idara ya usalama maeneo mbalimbali nchini katika shughuli ya sensa

Show More

Related Articles

Close