BiasharaMilele FmSwahili

Wabunge wa kike kupinga jaribio la kuwatimua waakilishi wakina mama bungeni

Wabunge wa kike wanasema watapinga jaribio lolote la kufutilia mbali nafasi za waakilisjhi akina mama katika bunge la kitaifa. Mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Vihiga Dorcas Kedogo na mwenzake wa Kakamega Rachel ameso wanasema jaribio la kufutilia mbali nafasi hizo ili kupunguza gharama ya serikali itakuwa kinyume na katiba. Wanasema nafasi hiyo ilibuniwa kwenye katiba ili kuwapa fursa akina mama kupata nafasi za uongozi. Pia wanataka kupitishwa kwa haraka kanuni zitakazofanikisha utekelezaji wa sheria kuhusu jinsia ili kuwapa wanawake zaidi nafasi za umma.

Show More

Related Articles

Close