HabariMilele FmSwahili

Wakenya 132 wamefariki kufikia sasa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi

Wakenya 132 wamefariki kufikia sasa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi. Serikali inasema wakenya elfu 330 wameathirika na mvua hii, kaunti 32 zikiwa ndio zimeathirika zaidi.

Ni mwezi wa pili sasa na mvua inayonyesha nchini imeendlea kuwapokonya wakenya maisha ikiwa waliofariki kufikia jana jioni ni 132.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna akitoa takwimu hizo anasema wakenya wengine elfu 17 hawana makao na mifugo wao wamefariki

Akidhibitisha hasara ambayo mvua hii imeacha, Oguna anasema mamlaka ya barabara kuu KENHA imeanza kutathmini hali

Ni hapa Oguna amewaomba wakenya wanaoishi maeneo ya chini na hatari kuhamia maeneo ya juu kuzuia maafa.

Wakati huo watu kadhaa wamefariki leo kaunti mbali mbali kutokana na mafuriko. Zaidi ya wenyeji 100 wamechwa bila makao eneo bunge la Keiyo Kusini na wengine 15 kaunti ya Muranga kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyoshuhudiwa maeneo hayo

Hali hii inashuhudiwa huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikidokeza mvua iliyonysha imezidi milimita 100 na inatarajiwa kunyesha mwezi huu wote wa Desemba.

Show More

Related Articles

Close