HabariMilele FmSwahili

Oguna : Watu 118 wamefariki kufikia sasa kutokana na athari za mafuriko nchini

Takriban wakenya 118 wamefariki kufikia sasa kufuatia mvua inayonyesha sehemu mbali mbali nchini. Idadi ya waliofariki kaunti ya Pokot Magharibi ikinakiliwa kuwa ya juu zaidi watu 43 wakifariki na maelfu ya wengine wakiachwa bila makao. Serikali inalenga kutumia shilingi bilioni 1 kununua misada ili kusambazwa katika maeneo yaliyoathirika.

Idadi serikali imenakili, ikiwa ni mwezi mmoja unusu tangu taifa kushuhudiwa mvua kubwa

Mafuriko yakiwa ndio matokeo, msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna anasema zaidi ya wakenya elfu 350 wameathirika vibaya na mvua hii

Kaunti ya Pokot Magharibi iliyokumbwa na janga kubwa zaidi ya ardhi kuporomoka, Oguna anasema hali hapa ni tete, miundu msingi ikiwa ndio inatatiza zoezi la usambazaji chakula

Akizungumza baada ya kuzuru kaunti hiyo, Oguna anasema wanahitaji shilingi bilioni 1 kuwafikia waathiriwa wote wa madhara ya mvua hii

Taarifa ya Oguna inawadia huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikionya kuanzia leo hadi mwanzoni mwa mwezi ujao wa desemba, mvua iliyozidi milimita 40 itashuhudiwa katika maeneo mengi ya nchini

Show More

Related Articles

Close