BiasharaMilele FmSwahili

Watu 24 wauwawa Somalia

Watu 24 wameuawa mjini baidoa kusini mwa Somalia walipokuwa wakitizama mechi baina ya Uanchester united na Aarsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na waasi wa Al shabab. Milipuko miwili ilitokea, katika mkahawa huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United na Arsenal. Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo. Mji wa baidoa ulinyakuliwa na waasi wa kundi la Al shabaab mwaka wa 2008,kabla ya kuondolewa mwaka 2012.

Show More

Related Articles

Close