HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya Kilo 100 za cocaine yenye dhamani ya shilingi milioni 598 zateketezwa katika makao ya DCI Nairobi

Zaidi ya kilo 100 za dawa za kulevya aina ya Cocain za dhamani ya shilingi milioni 598 zimeteketezwa leo katika makao makuu ya idara ya jinai DCI.

Zoezi hilo limeendeshwa kulingana na agizo la mahakama ya Milimani baada ya kesi iliyohusiana na dawa hizo kutamatika.

Shughuli hii iliyoagizwa na waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiangi na mkurugenzi wa DCI George Kinoti na jaji aliyeamrisha kuteketezwa dawa hizo Luca Kimaru ni mojapo wa mipango serikali imeweza kukabiliana na mihadarati nchini.

Dawa hizi zilinaswa Julai 29 mwaka 2016 katika kasha moja lililonaswa bandarini Mombasa likiwa limejaa dawa hizo.

Show More

Related Articles

Close