HabariPeople Daily

Wanafunzi Wakigeni Kutojiunga Na Shule Za Humu Nchini.

Serikali imepiga marufuku usajili wa wanafunzi wa kigeni katika shule ambazo ziko kwenye maeneo yanayokabiliwa na ukosefu wa usalama kama vile shule zilizopo kaunti ya Mandera.
Wizara ya elimu imetangaza kwamba hakutakuwa na usajili wa wanafunzi ambao wanatoka nchi jirani ya Somalia na nchi nyingine.
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Mandera Ismael Barrow amesema marufuku hiyo inafuatia agizo kutoka makao makuu ya wizara ya elimu.
Amesema wanafunzi wa mataifa ya nje ambao tayari wanaendeleza masomo katika shule za nchi hii wataendelea na masomo yao lakini watakuwa chini ya uangalizi.

Show More

Related Articles

Close