HabariPilipili Fm

Afisa Wa Polisi Mtekaji Nyara Kufikishwa Mahakamani.

Afisa mmoja wa polisi wa kitengo cha utawala ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi kwa madai ya utekeji nyara kijana wa umri wa mdogo.

Inaarifiwa kuwa maafisa wa kitengo cha flying squard walipashwa habari na wananchi na kuizuia gari ambayo ilikuwa inatumika na afisa huyo.

Afisa huyo alitumia gari aina ya probox yenye nambari ya usajili KBT 106W.

Akithibitisha kisa hicho kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohammed Maalim amesema sheria itachukua mkondo wake.

Mmiliki wa gari iliyo anazuiliwa na polisi huko likoni.

Washukiwa hao wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakama hivi leo.

Show More

Related Articles

Close