MichezoPilipili Fm

Bandari Kumthibitisha Odhiambo Kuwa Mkufunzi Wa Kudumu

Uongozi wa mabingwa wa Gotv  Bandari Fc umeonyesha kuridhishwa na matokeo mazuri yanayoandikishwa na timu hio baada ya kuondolewa kwa mkufunzi Twahir Muhiddin.

Yapata miezi miwili sasa tangu Muhiddin afukuzwe kazi kilabuni hapo na chini ya uangalizi wa kaimu mkufunzi Ken Odhiambo miamba hiyo ya pwani bado haijapoteza mechi hata moja kwenye mitinange mine ilyoshiriki hadi kufikia sasa.

Baada  tu ya kuondoka bandari muhiddin timu hio iliicharaza Ushuru nne mtungi na kutoka sare mbili dhidi ya Thika united na Homeboyz mtawalia na katika harakati za kutetea taji lao la gotv bandari waliiburuza na kufunza soka kwa kuitandika mabao 7 kwa nunge timu ya daraja la chini Tezo Fc.

Kulingana na Mohamed Abdulrahman Hassan anayeshughulikia maswala ya habari kilabuni hapo ni kuwa huenda Ken Odhiambo akathibitishwa kuwa mkufunzi wa kudumu kwani anaonekana kufanya kazi nzuri na kikosi cha Bandari.

Bandari kwenye mechi ya ligi kuu wikendi hii itapambana na Ushuru kwenye uga wa Mbaraki

 

Show More

Related Articles

Close