MichezoPilipili Fm

Bandari Yateua Afisaa Mpya Wa Habari

Mohammed Abdulrahman Hassan ameteuliwa kuwa afisaa wa kitengo cha habari katika kilabu ya bandari.

Uteuzi huu ulifanywa na bodi ya kilabu hio ya kanda ya pwani kwenye mkutano uliofanywa maalumu na kumwandikia Mohamed kuhusiana na uteuzi wake huo wa wadhfa huo kilabuni hapo.

Majukumu yake kama afisa wa habari atakua anahakikisha mkufunzi pamoja na wachezaji wanahudhuria vikao vya waandishi wa habarikwa mahojiano kwa wakati ufaao

Abdulrahman anachukua nafasi ya Ernest Mbalanya ambaye alihudumu hapo kwa muda wa miaka miwili.

Uteuzi huo ni moja ya malengo ya kilabu hio kufanya marekebisho huku mkufunzi mpya akiwa bado anasakwa kujaza pengo liloachwa na mkufunzi Twahir Muhiddin.

Show More

Related Articles

Close